• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Tanzania yatia saini mkataba wa kupatiwa fedha za msaada wa Sh60 bilioni kutoka Serikali China

    (GMT+08:00) 2019-06-25 18:45:21

    Tanzania imetia saini mkataba wa ku patiwa fedha za msaada wa Sh60 bilioni kutoka Serikali China bila ya masharti yeyote ambapo Serikali ya Tanzania itaamua matumizi yake katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wake.

    Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka Beijing China imesema mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Palamagamba Kabudi aliyeiwakilisha Tanzania na Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo la China Zhou Liujun kwa upande wa China.

    Mkataba huo umesainiwa punde tu mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya Waziri Kabudi na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi.

    Taarifa hiyo pia imetaja maeneo yatakayopewa kipaumbele kuwa ni pamoja na upembuzi yakinifu kwa ajili ya upanuzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ili kuwa Taasisi Mahiri ya Tiba ya Moyo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

    Mengine ni ujenzi wa mabwawa ya kuzalisha umeme ya Ruhudji (megawatt 358) na Rumakali (megawatt 222) mkoani yaliyoko mkoani Iringa na Njombe ambayo yote kwa pamoja yatakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa takribani megawati 580,pamoja na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge railway) sambamba na ukarabati wa reli ya Tazara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako