• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Tanzania laihimiza serikali kutoa tamko juu ya kauli za chuki zilizotolewa na mwanasiasa wa Kenya

    (GMT+08:00) 2019-06-26 09:04:16

    Spika wa Bunge la Tanzania Bw. Job Ndugai ameihimiza serikali kutoa tamko kuhusu usalama wa Watanzania nchini Kenya baada ya video inayomwonyesha mwanasiasa wa Kenya akitoa kauli za chuki kuenea katika mitandao ya kijamii.

    Video hiyo inamwonyesha mbunge wa Starehe nchini Kenya Bw. Charles Njagua Kanyi akichochea mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni wanaofanya kazi au biashara nchini humo.

    Bw. Ndugai amesema ingawa bado hajaona video hiyo, lakini anaamini kuwa serikali ya Tanzania inapaswa kutoa tamko kwa kuwa ni jambo la dharura.

    Katika video hiyo, Bw. Kanyi amesema hataki kuona wageni wanachukua fursa za wakenya za kufanya kazi na biashara, na kuipa serikali ya Kenya saa 24 kuwafukuza wageni hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako