• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AFCON: Nigeria waanza kuzua kizaazaa michuano ya Afcon baada ya kutolipwa posho

  (GMT+08:00) 2019-06-26 09:21:24

  Wachezaji wa Nigeria wapo kwenye mzozo na Chama cha Mpira wa Soka cha Nigeria (NFF) wakidhamiria kuigomea mechi yao ya leo dhidi ya Guinea kwenye michuano ya Kombe la Afrika nchini Misri. Hakuna hata mchezaji mmoja aliyelipwa posho yake au bonasi ya dola 10,000. Hata hivyo Chama cha Mpira wa Soka cha Nigeria kinataraji kuzuia mgomo huo kabla ya mechi hiyo kuchezwa. Kikosi cha kocha Gernot Rohr jana kilichelewa kwa saa nzima kufika mazoezini lakini hakijathibitisha kuwa kitachukua hatua zaidi. Chama hicho kinachopokea fedha kutoka serikalini, kimekataa kwamba kinahusika na uchelewashaji wa kuwalipa bonasi wachezaji wake. Kikosi cha Nigeria ambacho kimekusanywa tangu mwanzoni mwa Juni kimekuwa kikihakikishiwa kwa mdomo tu kuwa kitalipwa kabla ya mashindano kuanza mwezi huu. Hata hivyo kikosi hicho kimeamua kufuta mgomo wao na kuendelea na mzoezi yao kama kawaida.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako