• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapiga hatua katika juhudi za kuondoa umaskini kwenye sehemu zenye umaskini uliokithiri

    (GMT+08:00) 2019-06-26 17:07:48

    Ofisa mwandamizi wa ofisi ya kuwasaidia watu maskini iliyo chini ya baraza la serikali la China Bw. Ou Qingping amesema, China imeongeza nguvu katika kuondoa umaskini kwenye sehemu zenye umaskini uliokithiri, na hatua ijayo itakuwa ni kuhamasisha matumizi kuwa njia muhimu ya kuondoa umaskini.

    Kwa mujibu wa mpango wa kuondoa umaskini uliowekwa na serikali ya China, hadi kufikia mwaka 2020, China itawaondoa watu wote vijijini katika umaskini, na kuondoa umaskini uliokithiri kwenye wilaya zote. Naibu mkurungezi wa ofisi ya kuwasaidia watu kuondokana na umaskini iliyo chini ya baraza la serikali la China Bw. Ou Qingping amesema, sehemu zenye umaskini uliokithiri ni changamoto kubwa zaidi kwa juhudi ya kuondoa umaskini nchini China. Ameeleza kuwa mwaka 2017, China iliorodhesha wilaya 334 zenye umaskini uliokithiri, haswa katika mikoa mitano ya Tibet, Xinjiang, Sichuan, Yunnan na Gansu.

    Takwimu zinaonesha kuwa, kati ya mwaka 2018 hadi 2020, China imetenga zaidi ya dola bilioni 31 za kimarekani kwa ajili ya sehemu zenye umaskini uliokithiri, na nusu ya fedha hizo imetumiwa katika mikoa hiyo mitano. Bw. Ou amesema juhudi za kuondoa umaskini katika sehemu hizo zimepata ufanisi, akisema,

    "Mwaka jana tumewasaidia watu milioni 4.8 kuondokana na umaskini katika wilaya 334 zenye umaskini uliokithiri, ambao ni asilimia 38 ya watu wote walioondokana na umaskini nchini China mwaka huo. Hali hii inaonesha kuwa sera yetu inafanya kazi."

    Hata hivyo, Bw. Ou amesema juhudi za kuondoa umaskini bado zinakabiliwa na changamoto kubwa. Kwa mfano, katika mikoa mitano yenye umaskini zaidi, bado kuna watu milioni 1.72 wanaoishi kwenye umaskini uliokithiri, na kuwasaidia kuondokana na umaskini ni kazi ngumu.

    Alipozungumzia vigezo vya kuondokana na umaskini, Bw. Ou amesisitiza kuwa mstari wa mwisho ni hakuna shida ya kupata chakula, mavazi, elimu ya kimsingi, matibabu na makazi. Anaona kuwa kuwahamasisha watu maskini kuwa na hamu ya kuondokana na umaskini ni njia muhimu ya kupambana na janga hili.

    "Hadi kufikia mwaka 2020, endapo tutafanikiwa kuwasaidia watu wengi kuondokana na umaskini, huku watu wengi wakirejea kuwa maskini, hatuwezi kusema tumetimiza lengo letu. Ni lazima tuzingatie kazi ya kuimarisha matokeo ya kuondoa umaskini. Njia muhimu ni kuendeleza sekta za uchumi na kuhimiza ajira."

    Aidha, Bw. Ou amesema China itaongeza nguvu zaidi katika kupambana na umaskini katika siku zijazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako