• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika ni nguvu ya kuhimiza maendeleo ya dunia

    (GMT+08:00) 2019-06-26 18:55:33

    Mkutano wa waratibu wa kutekeleza matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC ulifungwa hivi karibuni hapa Beijing, na maonesho ya kwanza ya uchumi na biashara ya China na Afrika yatafunguliwa kesho mjini Changsha, China.

    Tangu mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC ufanyike mwezi Septemba mwaka jana, ushirikiano kati ya pande hizo mbili umepiga hatua kubwa zaidi, kwa mfano mazungumzo ya hatua ya kudumisha amani na usalama kati ya China na Afrika yalifanyika, China ilizindua taasisi ya utafiti wa mambo ya Afrika, na zaidi ya miradi 880 ya ushirikiano imeamuliwa kutekelezwa katika miaka mitatu ijayo.

    Kuinua kwa kiwango cha ushirikiano kati ya China na Afrika kwa mfululizo, si kama tu kunahitajiwa na maendeleo ya pande hizo mbili, bali pia kunalingana na mabadiliko ya hali ya kimataifa. Mwaka jana thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola bilioni 204.2 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 20 ikilinganishwa na mwaka 2017, na China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 10 mfululizo. Hadi sasa nchi 40 na kamati ya Umoja wa Afrika zimesaini makubaliano ya ushirikiano na China kufuatia pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Miradi ya ushirikiano kati ya China na Afrika ikiwemo reli inayounganisha Nairobi na Mombasa nchini Kenya, na eneo la ushirikiano wa uchumi na biashara la Suez nchini Misri, imechangia maendeleo ya jamii na uchumi barani Afrika.

    Hivi sasa, dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita, na nchi zinazoendelea zimedumisha maendeleo ya kasi. Ushirikiano kati ya China na Afrika utatoa mchango muhimu kwa ajili ya kuhimiza maendeleo zaidi ya nchi zinazoendelea, kuunda uhusiano mpya wa kimataifa na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, na utakuwa nguvu ya kuhimiza maendeleo ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako