• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa mwandamizi ahutubia Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya ulinzi wa haki za binadamu mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2019-06-26 19:14:39

    Mkoa unaojiendesha wa kabila la wa-uygur wa Xinjiang umepata maendeleo makubwa kuhusu ulinzi wa haki za binadamu na kutoa elimu ya mafunzo kazi ili "kuwalinda na kuwaokoa" watu walioshawishiwa na msimamo mkali wa kidini.

    Naibu Mkuu wa serikali ya mkoa huo ambaye ni m-uygur Bw. Aierken Tuniyazi ameongea mbele ya wajumbe 500 kwenye mkutano wa 41 wa baraza la haki za binadamu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

    Amewaambia wajumbe hao kuwa tangu miaka ya 90 hadi mwaka 2016, maovu matatu ya ubaguzi wa kidini, siasa kali za kidini na ugaidi, yamepangwa na kutekeleza matukio ya ugaidi na vurugu mkoani Xinjiang kutoka ndani na nje ya China, na kuleta madhara ya jamii ya huko.

    Amesema kwa kuanzisha elimu ya ufundi kazi na vituo vya mafunzo kwa mujibu wa sheria, wana lengo la kuwaelimisha na kuwaokoa wale walioshawishiwa siasa kali za kidini na kufanya makosa madogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako