• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eximbank ya China kutoa msaada wa kifedha kwa sekta binafsi Rwanda

    (GMT+08:00) 2019-06-26 19:20:06

    Benki ya Exim ya China imeonyesha nia ya kutoa msaada wa kifedha kwa sekta binafsi Rwanda.

    Hii ni kulingana na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi Rwanda Uzziel Ndagijimana.

    Ndagijimana aliyasema haya baada ya mkutana na maafisa wa Benki ya Exim mjini Beijing.

    Waziri Ndagijimana alikuwa China ambapo alijumuika na maafisa wengine 80 kutoka Afrika katika mkutano wa kufuatilia utekelezaji wa hatua za mkutano wa kilele FOCAC kati ya China na Afrika.

    Mkutano wa siku mbili wa Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) umetajwa na wajumbe kama fursa muhimu ya kubadilishana uzoefu kuhusu mahusiano kati ya China na Afrika,changamoto zilizopo na jinsi ya kuimarisha ushirikiano kwa ajili ya maslahi ya pande zote.

    Ndagijimana alisema kujitolea kwa Eximbank ya China kutoa msaada wa fedha kwa sekta binafsi kutasaidia sekta hiyo kuboresha biashara ya uagizaji na uuzaji nje bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako