• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa wapongeza vikosi vya Umoja wa Afrika kwa kuituliza Somalia

    (GMT+08:00) 2019-06-26 19:32:12

    Mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Bw. James Swan ambaye alifika jana Mogadishu, amepongeza mchango uliotolewa na vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Somalia kutokana na juhudi zinazoendelea kuituliza Somalia.

    Bw. Swan ameahidi kushirikiana na tume ya Umoja wa Afrika (AMISOM) kusaidia kuunga mkono juhudi za amani nchini Somalia. Amesema Umoja wa Afrika ni mshirika muhimu wa Umoja wa Mataifa.

    Bw, Swan ameteuliwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Gutteres kukutana na maofisa waandamizi wa AMISOM wakiongozwa na mwakilishi maalum wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Fracisco Madeira kwenye kazi yake ya kwanza nchini Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako