• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China ajibu barua kwa kijana wa Japan

  (GMT+08:00) 2019-06-26 19:56:07

  Rais Xi Jinping wa China amejibu barua kutoka mshindi wa mashindano ya Kombe la Panda ya insha ya vijana wa Japan Bw. Nakajima Daiiti, ambaye amemwandikia barua na kumtakia rais Xi kila la heri, na kuonesha matarajio mema ya kazi za urafiki kati ya China na Japan.

  Kwenye barua yake, rais Xi amesema anafurahia Bw. Daiiti kujifunza lugha na fasihi ya kichina kwa muda mrefu, na kushiriki kwa hamu kubwa kwenye mashindano hayo ili aielewe zaidi China na kuimarisha urafiki na marafiki wa China. Anatarajia Bw. Daiiti atashiriki zaidi kwenye mambo ya urafiki kati ya pande hizo mbili.

  Rais Xi pia amesema vijana ni watu muhimu katika kuendeleza urafiki baina ya nchi hizo mbili. Anatarajia kuwa vijana wa nchi hizo mbili wataongeza mawasiliano, maelewano na kuendeleza urafiki wa muda mrefu, ili kutoa mchango katika kujenga mustakabali mzuri zaidi wa uhusiano kati ya China na Japan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako