• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Zinedine Zidane apania kurudisha mtindo wa samba kwenye Real Madrid

  (GMT+08:00) 2019-06-27 14:20:47

  Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amepania kuona timu yake ikicheza soka ya kuvutia ya pasi aina ya samba ambayo huchezwa zaidi nchini Brazil. Zidane anaamini katika siku za karibuni Real Madrid imekuwa haivutii katika uchezaji wake. Dalili za hali hiyo ni kitendo chake cha kumsajili dogo wa kibrazili, Rodrygo kwenye kikosi chake. Rodrygo ameweka rekodi ya kuwa nyota wa 26 wa kibrazili kuwahi kuchezea Real Madrid ambayo ilianzishwa miaka 117 iliyopita. Zidane sasa amepania kuona timu yake ikicheza soka safi ya pasi ambayo huko Brazil huitwa samba ili kuweza kuvutia duniani kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako