• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Bilionea wa Uingereza Jim Ratcliffe aimendea klabu ya Manchester United

  (GMT+08:00) 2019-06-27 14:21:13

  Jim Ratcliffe, ambaye ndiye tajiri zaidi nchini Uingereza, anaripotiwa kuwa na azma ya kuinunua klabu ya Manchester United kutoka kwa Wamarekani Glazer. Shabiki huyo mkubwa wa klabu hiyo tangu utotoni, anamiliki mali inayaogharimu pauni bilioni 21, na pia alikuwa na lengo hilo moja la kuitaka klabu ya Chelsea mapema mwaka jana. Tajiri huyo ambaye ni mfadhili wa timu ya Uingereza ya waendesha baiskeli, Ineos, hutoa mfukoni mwake takriban pauni milioni 40 kila mwaka kufadhili kikosi hicho. Klabu hiyo ya Old Trafford inagharimu pauni bilioni 3.8 na mashabiki wake wanataka Glazers kuiuza. Gharama hiyo ni ishara tosha kwamba Ratcliffe atalazimika kuuza sehemu kubwa ya mali yake ili kutuliza kiu yake ya kutaka kuwa mumiliki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako