Kocha wa timu ya taifa ya Misri, Hani Abu Reda ametangaza kumtimua kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Amr Medhat Warda. Warda mwenye umri wa miaka 25, ametemwa ikiwa ni masaa machache kabla ya mchezo wa pili wa hatua ya makundi katika michuano ya AFCON inayoendelea nchini humo, mchezo ambao ilipigwa jana dhidi ya Congo DR majira ya saa 5:00 usiku na Misri kujinyakulia nafasi kwenye nafasi ya 16 bora baada ya kuwakandamiza wageni wao kwa mabao 2-0. Imetajwa kuwa nidhamu mbovu ndiyo sababu za kuachwa kwake, ambapo kwa mujibu wa mitandao mbalimbali nchini Misri, mchezaji huyo amehusika katika unyanyasaji dhidi ya mwanamitindo raia wa nchi hiyo, Merhan Keller. Warda ni kiungo mshambuliaji katika klabu ya PAOK ya nchini Ugiriki.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |