• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga vitendo vya kujilinda kibiashara huku ikifungua mlango zaidi

    (GMT+08:00) 2019-06-27 18:05:07

    Kutokana na vitendo vya kujilinda kibiashara vinavyoendelea hivi sasa, uchumi wa dunia unakabiliwa na changamoto kubwa. Dunia nzima inatarajia kuwa mkutano wa kilele wa Kundi la Nchi 20 (G20) utakaofanyika mjini Osaka, Japan utaonesha msimamo wazi wa kupinga vitendo hivyo, ili kurejesha uchumi wa dunia kwenye njia sahihi ya maendeleo.

    Mwaka 2013, kiongozi wa China alitoa pendekezo la "kuunda uchumi wa dunia unaofungua mlango", ambalo linaendana na mkondo wa maendeleo ya zama hii na matumaini ya watu wa nchi mbalimbali. Na katika miaka kadhaa iliyopita, China imefanya juhudi kubwa ili kutimiza lengo hilo.

    Mwezi Machi mwaka huu, China ilipitisha sheria ya uwekezaji kutoka nje, ili kufungua mlango zaidi. Takwimu zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu, China ilitumia uwekezaji wa nje wenye thamani ya karibu dola bilioni 54 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 6.8 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Sera ya kufungua mlango zaidi ya China si kama tu imekaribishwa na wawekezaji wa nchi za nje, bali pia imezinufaisha nchi zinazoendelea. Mkurugenzi wa Shirika la Development Reimagined Bi. Hannah Wanjie Ryder amesema, mwaka 2000, oda ya bidhaa za China kutoka nchi nyingine zisizo za Afrika ilikuwa mara 44 ya oda kutoka nchi za Afrika, lakini sasa ni mara 22 tu, wakati huohuo, oda ya bidhaa ya Marekani kutoka nchi zisizo za Afrika ni mara 70 ya oda zake kutoka nchi za Afrika. Amehimiza nchi zilizoendelea kuiga mfano wa China, na kuisaidia Afrika kujiunga na mchakato wa maendeleo ya uchumi wa dunia.

    Kuna methali moja inayosema, "mtu akiwa peke yake anatembea haraka, lakini wakiwa wengi wanafika mbali". Vitendo vya kujilinda kibiashara vinaweza kuisaidia nchi kupata maendeleo ya kasi, lakini madhara yanayosababishwa na vitendo hivyo kwa nchi nyingine, hatimaye yataathiri maendeleo ya nchi hiyo yenyewe.

    Mtafiti wa juu wa Chuo Kikuu cha Cambridge cha Uingereza Bw. Martin Jacques anaona vitendo vya kujilinda kibiashara vya Marekani na sera yake ya "Marekani kwanza" vinaonekana kama vinaonesha nguvu ya Marekani, lakini kwa kweli vimedhihirisha udhaifu wa nchi hiyo. Mwelekeo wa mafungamano ya uchumi wa dunia hauzuiliki, nchi wanachama wa Kundi la Nchi 20 zinapaswa kushikilia hatua zilizothibitishwa kuweza kuhimiza maendeleo ya uchumi wa dunia, haswa utaratibu wa pande nyingi.

    Wakati wa mkutano wa kilele wa Kundi la Nchi 20, kiongozi wa China atakutana na viongozi wa nchi mbalimbali, ili kubadilishana nao maoni kuhusu juhudi za kulinda utaratibu wa pande nyingi, na kuhimiza uchumi wa dunia unaofungua mlango. Kwenye mkutano huo, China itaendelea kuchangia busara kwa ajili ya kukamilisha usimamizi wa mambo ya kimataifa, kama ilivyofanya katika mikutano iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako