• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TWENZETU AFCON 2019: Ilikuwa ni Do or Die "Kufa ama kupona" Tanzania yaangukia pua kwa majirani zao Kenya

  (GMT+08:00) 2019-06-28 08:52:55

  Ilikuwa majira ya saa tano usiku kwa saa za Afrika Mashariki jana, wakati majirani wawili wa Afrika Mashariki, Taifa Stars ya Tanzania ilipovaana na Harambee Stars ya Kenya katika mchezo uliokuwa ukitabiriwa na wengi kuwa mkali.

  Timu hizo ziliingia uwanja wa Juni 30 jijini Cairo Misri ikiwa ni mwendelezo wa michezo ya kundi C kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika (AFCON 2019). Timu hizo ziliingia uwanjani zikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza michezo yao ya kwanza, ambapo Tanzania ilipoteza kwa Simba wa Teranga ya Senegal kwa goli 2-0, huku Kenya wakipoteza kwa Algeria kwa idadi hiyo hiyo ya magoli.

  Bao la pekee la Mohamed Belaili limetosha kuipa ushindi wa 1-0 Algeria dhidi ya Simba wa Teranga Senegal na kuifanya timu hiyo kutangulia 16 bora ya kombe hilo la mataifa ya Afrika, huku Tanzania wao wakifungashiwa virago jana na Kenya. Timu zingine zilizotinga hatua ya 16 bora ni wenyeji Misri na Nigeria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako