Michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki ama Kombe la Kagame litaanza kutimua vumbi Julai 7 mjini Kigali Rwanda, mabingwa watetezi Azam FC ya Tanzania itaanza kampeni zake za kutetea ubingwa huo kwa kupambana na Mukura Victory ya Rwanda.
Mechi zingine zitakazopigwa siku hiyo ni Bandari ya Kenya itakutana na KCCA ya Uganda, huku KMC ya Tanzania itavaana na Atlabara ya Sudan Kusini, na Rayon Sports ya Rwanda itakutana na TP Mazembe ya DRC. Wawakilishi wa Zanzibar KMKM wao watashuka dimbani Julai 8 kuvaana na AS Ports ya Djibouti.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |