Kiungo wa kati wa mabingwa wa mpira wa kikapu wa NBA Toronto Raptors, Marc Gasol amebakizwa kuendelea kuchezea timu hiyo kwa msimu ujao wa 2019/20, taarifa zilizotolewa na klabu hiyo imebainisha.
Gasol alitumikia ligi hiyo kwa miaka 10 akiwa na klabu ya Memphis kabla ya kuhamia Raptors, atakuwa akilipwa kitita cha dola za Marekani 25,595 na 700.
Gasol aliisaidia timu yake ya Raptors katika mechi mbili muhimu zilizoipatia ubingwa, moja ilikuwa kati ya Toronto Raptors dhidi ya Golden State Warriors na mchezo mwingine ulikuwa kati ya Raptors dhidi ya Bucks ambazo zilikuwa wapinzani wake wakubwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |