Watoto wa darajani Stamford Chelsea inadaiwa imezigomea vilabu vya Barcelona na Atletico Madrid zinazomgombea winga wake, Willian.
Klabu hiyo inaaminika kuwa imekataa kumwachia winga huyo baada ya kumpoteza Eden Hazard, ambaye alijiunga na Real Madrid hivi karibuni.
Willian mwenye umri wa miaka 30 anatazamiwa kumaliza mkataba wa kuchezea timu hiyo baada ya kumalizika msimu wa 2019/20.
Chelsea imeweka ngumu kumuuza Willian kutokana na ukweli kuwa wamempoteza Hazard na pia wamefungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). Barcelona ndio timu ambayo kwa muda mrefu zaidi imekuwa inamwania Willian.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |