• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kuangalia namna ya kuwezesha kifedha wadau wanaofanya tafiti

    (GMT+08:00) 2019-06-28 18:41:55

    Serikali ya Tanzania imesema itaangalia namna ya kuwezesha kifedha wadau wanaofanya tafiti ili kuhakikisha matokeo ya tafiti hizo yanaunganishwa na viwanda.

    Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Dk Leonard Akwilapo amesema tafiti nyingine zinaishia kwenye machapisho lakini sasa Serikali ya Tanzania inajitahidi kuhakikisha yale ambayo wanagundua katika tafiti yanaunganishwa na viwanda ili kuunga mkono sekta hiyo.

    Amesema viwanda vingi vinaletwa na watu kutoka nje hivyo wanazalisha kwendana na teknolojia yao, hivyo ili kukomesha hali hiyo ni Serikali kuwa na vyanzo vya fedha kwa ajili ya kuanzisha viwanda vitakavyotumia teknolojia ya ndani na tafiti zilizofanywa na wataalamu wa nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako