• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mzaha wa kupeleka mizigo Nairobi na kuirejesha Mombasa

    (GMT+08:00) 2019-06-28 18:44:22

    Wafanyabiashara jijini Mombasa wanaoagiza bidhaa kutoka ng'ambo, wamelalamikia hatua ya serikali kuwaagiza kusafirisha mizigo yao hadi Nairobi kukaguliwa na kulipia ushuru na kisha kuisafirisha tena hadi Mombasa.

    Wafanyibishara hao wanasema hatua hiyo itaongeza gharama ya kufanya biashara.

    Wamesema hawaelewi sababu za kupeleka shehena zao hadi kituo cha Inland Container Depot jijini Nairobi kwa reli ya kisasa (SGR) licha ya mizigo hiyo kuandikishwa kuwa ni ya Mombasa.

    Baadhi yao wamelazimika kulipa zaidi ya Sh109,446 za kuhifadhi shehena Nairobi, ada ya SGR na gharama ya kurudisha mizigo yake hadi Mombasa. Stakabadhi zilizodhihirisha shehena hizo kupelekwa Nairobi zinaonyesha kuwa wafanyibiashara hao watalazimika kulipia kati ya Sh70,000 na Sh120,000 kama ada inayotozwa mizigo kuhifadhiwa zaidi ya siku nne eneo la ICD.

    Mwaka uliopita, Shirika la Reli nchini lilitangaza kuwa mizigo yote itakayoagizwa kutoka ng'ambo itasafirishwa kwa SGR hadi Nairobi ili kuongeza mapato ya shirika hilo linalodaiwa zaidi ya Sh327 bilioni na serikali ya China kwa kujenga SGR.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako