• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiwanda cha Rivatex chaleta matumaini

    (GMT+08:00) 2019-06-28 18:44:43

    Kufufuliwa kwa kiwanda cha kutengeneza nguo cha Rivatex kumewapa matumaini mapya wakulima wa pamba kutoka iliyokuwa mikoa ya Nyanza, Bonde la Ufa na Magharibi.

    Kiwanda hicho kilichofunguliwa upya na Rais Uhuru Kenyatta Ijumaa iliyopita kilisifika miaka ya themanini na tisini kwa kutengeneza nguo na kubuni nafasi nyingi za ajira kwa Wakenya.

    Wakulima wa pamba katika eneo hilo wamesema ni vyema kuhakikisha kwamba matatizo yaliyoizonga Rivatex miaka ya nyuma na kusababisha kuporomoka kwake hayarejelewi tena.

    Hata hivyo, ufanisi huo utafikiwa tu iwapo serikali itatekeleza mikakati kadhaa ambayo ikitiliwa manani basi kiwanda hicho kitafanikisha maazimio yake.

    Baadhi ya viongozi wa eneo hilo wamesema serikali inafaa kuhakikisha kwamba maafisa wakuu wa kiwanda hicho ni watu wenye maadili na wasiojawa na tamaa ya kufuja mali ya umma wakiwa uongozini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako