• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atangaza hatua tano muhimu za China kwenye Mkutano wa kilele wa G20

    (GMT+08:00) 2019-06-28 20:30:08

    Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba muhimu kuhusu kushirikiana katika kujenga uchumi wa dunia wenye ubora wa hali ya juu kwenye Mkutano wa kilele wa kundi la nchi 20 G20 unaofanyika nchini Japan.

    Kwenye hotuba yake, rais Xi ametangaza hatua tano muhimu zitakazochukuliwa na China, ili kujenga hali mpya ya ufunguaji mlango na kujitahidi kutimiza maendeleo yenye ubora wa juu.

    Hatua hizo mpya ni pamoja na kufungua zaidi soko kwa nje, kuongeza uagizaji bidhaa kutoka nje, kuendelea kuboresha mazingira ya biashara, kuyatendea kwa usawa mashirika yote yaliyoandikishwa nchini China na kuongeza nguvu ya kuhimiza mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako