• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Marekani wakutana

    (GMT+08:00) 2019-06-29 19:41:22

    Rais Xi Jinping wa China na leo amekutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Marekani Donald Trump pembeni ya mkutano wa kundi la nchi ishirini G20 mjini Osaka Japan, na kukubaliana kuanzisha tena mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya nchi zao kwa msingi wa usawa na kuheshimiana.

    Upande wa Marekani umesema hautaongeza ushuru mpya wa forodha kwa bidhaa za China, na pande mbili zitajadili mambo mahsusi.

    Mwanzoni mwa mkutano wao Rais Xi amesema, licha ya mabadiliko makubwa yaliyotokea katika hali ya kimataifa na kwenye uhusiano kati ya China na Marekani katika miaka 40 iliyopita, kitu kimoja cha msingi ambacho hakijabadilika, ni kuwa China na Marekani zote zinanufaika na ushirikiano na zinapoteza kutokana na migongano. Amesema ushirikiano na mazungumzo ni bora kuliko mivutano na migongano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako