Taarifa ya afisa habari na mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo imesema dirisha la usajili litafungwa Julai 31, mwaka huu na hakutakuwa na muda wa ziada baada ya zoezi hilo kufungwa.
Taarifa hiyo imesema kwamba usajili wa mashindano ya CAF kwa Klabu za Simba, Yanga SC, Azam FC na KMC wenyewe utafungwa Julai 10, mwaka huu.
Simba na Yanga wanawakilisha nchi hiyo kwenye ligi ya mabingwa Afrika, wakati Azam FC na KMC wanawakilisha kwenye kombe la shirikisho na TFF imesisitiza vilabu vyote kufanya usajili kwa wakati.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |