• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TWENZETU AFCON 2019: Tanzania kwaheri, Kenya yasubiri, zalazwa na Algeria na Senegal

  (GMT+08:00) 2019-07-05 09:54:31

  Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kimekamilisha rasmi safari ya michuano ya AFCON huko Misri kwa kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Algeria.

  Katika mchezo huo wa kundi C, Stars imepokea kichapo cha tatu mfululizo baada ya kufungwa na Senegal kwa mabao 2-0 kisha Kenya kwa mabao 3-2.

  Mabao ya Algeria usiku huu yamewekwa na Islam Silmani pamoja na Adam Ounas aliyeingia kambani mara mbili.

  Wakati huo huo, mshambuliaji wa Liverpool ya Uingereza raia wa Senegal Sadio Mane, ameifungia Senegal bao moja na kuisaidia timu yake kuchukua nafasi ya pili katika kundi C baada ya kuilaza Kenya 3-0 na kufuzu miongoni mwa timu 16 bora.

  Kenya inaweza ikafuzu kama timu ya tatu bora ikitegemea matokeo katika mechi ya mwisho katika kundi E and F. Hata hivyo matokeo ya Jumatatu yanamaanisha kwamba DR Congo inaweza kufuzu kutoka kundi A ikiwa na goli moja zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako