• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuendeleza uhusiano kati ya China na Marekani ni matarajio ya watu wa nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2019-07-02 09:56:44

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang jana amesema, mrejesho kuhusu mkutano kati ya wakuu wa China na Marekani unaonyesha kuwa, kuendeleza uhusiano kati yao ni matarajio ya watu wa nchi hizo mbili, pia ni matarajio ya jumuiya ya kimataifa.

    Bw. Geng Shuang amesema, wakuu wa China na Marekani wamefikia makubaliano muhimu, ikiwemo kuendelea kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili ambao una msingi wa uratibu, ushirikiano na utulivu, na pande mbili hizo zimetangaza kuanzisha tena mazungumzo ya uchumi na biashara kwenye msingi wa usawa na kuheshimiana. Makubaliano hayo yameeleza mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano huo katika kipindi kijacho, na kuleta mwitikio mzuri katika nchi hizo mbili na jumuiya ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako