• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China tayari kufadhili ujenzi wa SGR asema waziri wa fedha wa Uganda

    (GMT+08:00) 2019-07-02 19:56:08
    Waziri wa fedha wa Uganda Matia Kasaija amesema China siku zote imekuwa tayari kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa nchini Uganda lakini kumekuwa na ucheleweshaji kutokana na mchakato wa maelewano kati ya Kenya na Uganda.

    Kasaija amesema hayo baada ya kurejea kutoka ziarani nchini China ambapo alihakikishiwa na serikali ya China kuwa ufadhili wa reli ya kisasa utatolewa pindi tu Kenya na Uganda zitakapomaliza mazungumzo.

    Kenya inatarajiwa kujenga reli yake hadi eneo la mpakani la Malaba ili kuungana na Uganda.

    Waziri kasaija pia amesema rais Yoweri Museveni, waziri wa uchukuzi wa Kenya James Macharia na waziri wa biashara wa China pamoja na maafisa wa benki ya EXIM ya china walifanya mkutano mjini Beijing kujadili hali ya baadaye ya kutolewa kwa ufadhili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako