• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya maendeleo ya kilimo ya Tanzania kusaidia ukusanyaji wa kahawa kwa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-07-02 20:43:48
    Msimu wa ukusanyaji wa kahawa kwa mwaka 2019/2020 kutoka kwa wakulima hadi vyama vya msingi umezinduliwa rasmi mkoani Kagera, huku Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ikiwahakikishia wakulima wa zao hilo kupata malipo yao kwa wakati.

    Katika msimu uliopita Benki ya Maendeleo ya Kilimo ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 30 ambazo ziliwanufaisha moja kwa moja wakulima 148,000.

    Akizungumza baada ya kuzinduliwa msimu wa ukusanyaji wa kahawa ambapo vyama vikuu vya ushirika vya KCU 1990 na KDCU kutangaza malipo ya awali kuwa shilingi 1,100 kwa kilo moja ya maganda, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine, amesema benki yake itatoa fedha kwa wakati na kumfikia mkulima moja kwa moja kupitia mfumo wa benki.

    Justine aliwathibitishia wakulima kuwa TADB imejipanga kimkakati kuhakikisha kuwa wakulima wananufaika na kuwapo kwa benki ikiwamo kupata malipo yao kwa wakati na kumudu kununua pembejeo za kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako