• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Michuano ya kanda ya tano, Misri wazua tafrani

    (GMT+08:00) 2019-07-03 08:56:44
    Wakati mchezo wa mpira wa kikapu kati ya Tanzania dhidi ya Kenya upande wa wanaume michuano ya kikapu kanda ya tano ukichezwa mwishoni mwa wikiendi kwenye uwanja wa Lugogo, Kampala nchini Uganda, wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Misri walitia aibu kwa kuzua vurugu kubwa.

    Vurugu hizo zilizosababisha mchezo huo kusimama kwa zaidi ya dakika tatu, zilitokana na baadhi ya wachezaji hao wa Misri kutaka kuchukua viti ambavyo vilikuwa kwenye benchi la timu ya Taifa ya Tanzania.

    Baada ya dakika chache kupita, vurugu zilisimama na kila mmoja kurudi nafasi yake, kisha wachezaji wa Misri wakatengewa viti vyao na kuendelea kufuatilia mchezo huo, ambapo hadi mchezo unamalizika Tanzania ilipoteza kwa pointi 112-74 dhidi ya Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako