• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kombe la Copa America- Brazil uso kwa uso na Argentina

    (GMT+08:00) 2019-07-03 08:57:26
    Ulimwengu wa soka utasimama leo Jumatano pale watani wa jadi Brazil na Argentina watakapokuwa wanakwaana katika nusu fainali ya taji la kuwania ubingwa wa Amerika Kusini Copa America.

    Tambo kutoka pande zote tayari zimeanza kurushwa kuelekea mchuano huo wa kukata na shoka. Mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus amesema, Argentina watakuwa na wakati mgumu kuivunja safu yao ya ukabaji kwa kuwa katika mechi nne walizocheza hawajakubali goli langoni mwao.

    Iwapo Argentina watafuzu kwenye fainali na kushinda basi watakuwa wameifikia rekodi ya Uruguay ya kushinda mataji 15 ya mashindano hayo ya Copa America.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako