• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kombe la dunia la wanawake- Marekani yafanya kweli

  (GMT+08:00) 2019-07-03 08:59:37

  Mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia la wanawake umepigwa jana Jumanne jijini Lyon Ufaransa, hadi kipenga cha mwisho cha refa, Marekani wameibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Uingereza.

  Leo ni zamu ya Uholanzi kupimana ubabe na Uswidi katika mchezo wa nusu fainali nyingine.

  Uingereza ambao wanashika nafasi ya tatu duniani hawajawahi kufanikiwa kupita hatua ya nne bora misimu minne iliyopita ya fainali za kuwania ubingwa wa kombe la dunia.

  Kwa upande wa Marekani, ambao ni mabingwa mara tatu wa Kombe la dunia wanajivunia rekodi bora zaidi dhidi ya Uingereza. Miamba hao wa soka wamepoteza mechi moja pekee kati ya tano zilizopita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako