• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Bei za mafuta, pombe, sigara na pikipiki kuongezeka

    (GMT+08:00) 2019-07-03 19:47:58
    Bei za mafuta, pombe, sigara na pikipiki zinatarajiwa kuongezeka huku Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA) ikianza kutoza ushuru wa asilimia 5.17 wa marekebisho ya kodi ya mfumuko wa bei.

    Utekelezaji wa marekebisho ya kodi ya mfumuko wa bei, ulianza kwanza mwaka jana lakini ukasimamishwa kwa miaka mitatu, lakini sasa unatarajiwa kuanza upya kuanzia wakati wowote.

    Sheria inasema kuwa KRA inapaswa kufanya marekebisho mwanzoni mwa mwaka wa fedha, ambayo ni Juali 1.

    Waziri wa fedha Henry Rotich analenga ongezeko la Sh37 bilioni kutokana na kodi mpya kutokana na makadirio ya kodi ya Sh1.8 trillion ambayo KRA inatarajiwa kukusanya mwaka huu wa kifedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako