• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: AFCON 2019: Ratiba ya hatua ya mtoano hadharani

    (GMT+08:00) 2019-07-04 08:23:42
    Ratiba ya hatua ya mechi za mtoano, ama 16 bora ya AFCON tayari ipo wazi. Mwakilishi pekee wa Afrika Mashariki aliyebaki katika mashindano hayo Uganda imeangukia mikononi mwa Simba wa Teranga ya Senegal toka Afrika Magharibi na watakipiga kesho Ijumaa usiku kwenye uwanja wa kimataifa wa Cairo, Morocco watavaana na Benin.

    Jumamosi Julai 6, Nigeria watakutana na Cameroon huku wenyeji Misri watakutana na Afrika Kusini. Na Jumapili Julai 7, Madagascar watawavaa DR Congo, nao Algeria watatoshana nguvu na Guinea. Na jumatatu Mali wao watacheza na Ivory Coast, huku Ghana uso kwa uso na Tunisia.

    Mbali na timu zilizofuzu kutokana na kushinda mechi zao, timu nne pia zimefuzu katika raundi ya mtoano kama timu bora kati ya wale walioshindwa. Mataifa hayo ni Guinea, DR Congo, Afrika Kusini na Benin.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako