• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Palestina asema Marekani haijafanya kitu chochote kwa ajili ya amani

    (GMT+08:00) 2019-07-04 10:00:19

    Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesema Marekani haijafanya kitu chochote katika kuhimiza mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa Amani wa Oslo mwaka 1993. Abbas amewaambia wanahabari katika mji wa Ramallah, Ukingo wa Magharibi kuwa watu wa Palestina hawakubali Marekani kuwa mpatanishi wa mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel na kwamba mbali na kundi la pande nne la amani ya Mashariki ya Kati linaloundwa na Marekani, Russia, Umoja wa Mataifa na Ulaya, China, Japan na nchi nyingine za kiarabu pia zinaweza kuwa wapatanishi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako