Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ,Isaac Kamwelwe,jijini Dar es Salaam ,akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wake wachimbaji wakubwa wa madini duniani na wafanyabiashara waliokutana kwa lengo la kujadili changamoto zinazokwamisha kupitisha mizigo katika bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia 100 na kiwango cha utoaji mizigo ni asilimia 25 hadi 40.
Kamwelwe alisema ili kumaliza changamoto hiyo,ameshamwandikia barua Waziri wa Fedha na Mipango,Dk Philip Mpango ,ili watumishi wa wizara hiyo wafanye kazi katika bandari hiyo yenye jengo linaloweza kutoshea watumishi wa idara zote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |