• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wang Yi akutana na mwenyekiti mteule wa Baraza kuu la awamu 74 la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2019-07-04 19:44:03

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Bw. Wang Yi leo hapa Beijing amekutana na mwenyekiti mteule wa Baraza kuu la awamu 74 la Umoja wa Mataifa Bw. Tijjani Muhammad-Bande.

    Bw. Wang amempongeza Bw. Bande kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa awamu mpya wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa. Amesema, hivi sasa vitendo vya upande mmoja, kujilinda kibiashara, na vitendo vya umwamba vinaleta athari mbaya na changamoto kwa utaratibu wa kimataifa, pande mbalimbali zinataka mjadala wa kawaida wa Baraza kuu wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwezi wa Septemba mwaka huu kutoa sauti ya pamoja kuunga mkono mfumo wa pande nyingi na kuimarisha mchango wa Umoja huo. China inapenda kuunga mkono na kushirikiana na baraza hilo kupata maendeleo katika maendeleo endelevu, mabadiliko ya hali ya hewa, haki za wanawake na vijana, amani na usalama wa kimataifa.

    Bw. Bande amesema jumuiya ya kimataifa inahitaji zaidi mfumo wa pande nyingi kuliko zamani, huku akiishukuru China kwa uungaji mkono wa siku zote kwa kazi za baraza kuu hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako