• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Licha ya kupoteza mechi zote, Tanzania yapewa tuzo

    (GMT+08:00) 2019-07-05 09:52:24
    Licha ya kufungwa mechi zote katika mashindano ya Afrika ya mchezo wa kikapu kanda ya tano, Tanzania imetwaa tuzo mbili katika mashindano hayo nchini Uganda.

    Nyota wa Tanzania, Baraka Athman ni miongoni mwa wachezaji waliizoa tuzo ya ufungaji bora katika mashindano hayo.

    Mbali na tuzo ya mfungaji bora, pia Tanzania imetwaa tuzo ya timu iliyoonyesha mchezo wa kiungwana yaani fair play. Tuzo ya mchezaji bora imeenda kwa Brandon Davies wa Uganda na kinara wa MVP wa mashindano hayo ni Tyler Ongwae wa Kenya.

    Kenya imetwaa ubingwa ikimtoa bingwa mtetezi Misri aliyeambulia nafasi ya pili na Uganda kukamata nafasi ya tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako