• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapongezwa kwa maendeleo mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2019-07-05 10:29:42

    Ujumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa mjini Geneva umefanya mkutano kuhusu "mafanikio ya maendeleo ya haki za binadamu mkoani Xinjiang", ambao umehudhuriwa na zaidi ya watu 160, wakiwemo wanadiplomasia wa nchi mbalimbali na maofisa wa mashirika ya kimataifa.

    Mjumbe wa kudumu wa China katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva Bw. Chen Xu amesema, hiki ni kipindi ambacho mkoa wa Xinjiang unaendelea kwa kasi na utulivu zaidi katika historia, na China imeweka kipaumbele katika maslahi ya kimsingi ya watu wa makabilia tofauti mkoani humo. Pia China inapambana na uhalifu wa kigaidi na kimabavu kwa kufuata sheria, huku ikitilia maanani kukinga ugaidi na kuondoa chanzo cha ugaidi, na imepata mafanikio mazuri.

    Wajumbe waliohudhuria mkutano huo wameipongeza China kwa kupata maendeleo makubwa katika uchumi na haki za binadamu, pamoja na mafanikio katika kupambana na ugaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako