• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka ya bandari Uganda kuanza kujenga miundo mbinu katika uwanja wa ndege wa Entebbe

    (GMT+08:00) 2019-07-05 17:34:30

    Mamlaka ya bandari nchini Uganda imesaini makubaliano na shirika la kitaifa la biashara nchini humo NEC kujenga awamu ya kwanza ya eneo huru la bandari katika uwanja wa ndege wa Entebbe. Makubaliano hayo yalisainiwa na katibu mkuu mtendaji wa Bandari nchini humo Bw Richard Jabo na mwenzake wa NEC Bw James Mugira.Mamlaka ya bandari ilipatiwa hekari 5 za ardhi na mamlaka ya safari za anga nchini humo kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya bandari huru mwaka wa 2018. Hii ni sehemu ya mpango wa kuboresha na kupanua bandari ya Entebbe.Bandari hiyo inbaratajiwa kuunda ajira 200 za moja kwa moja pindi itakapokamilika. Baadhi ya sekta zinazolengwa ni vyakula, maua miongoni mwa nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako