• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Familia za baadhi ya waathiriwa wa ajali ya ndege ya Boeing zakataa fidia

    (GMT+08:00) 2019-07-05 17:34:49

    Baadhi ya familia za watu waliopoteza wapendwa wao kwenye ajali ya ndege ya Boeing ilioanguka nchini Ethiopia wamesema hawatakubali fidia inayotolewa na kampuni hiyo ya ndege.

    Boeing inasema kuwa itatoa $100m kwa miaka kadhaa kwa serikali za mtaa na mashirika yasio ya kiserikali kuzisaidia familia na jamii zilizoathirika na ajali hiyo ya ndege aina ya 737 MAX nchini Indonesia na Ethiopia.

    Malipo hayo yatakayotolewa kwa miaka kadhaa hayatokani na kesi iliowasilishwa mahakamani baada ya ajali hiyo ambayo ilisababisha vifo vya takriban watu 346. Ajali hiyo ya mwezi Machi ilikuwa ya pili kuhusisha ndege ya Boeing aina ya 737 Max katika kipindi cha muda wa miezi mitano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako