• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara kati ya China na Afrika yaongezeka Januari hadi Mei

    (GMT+08:00) 2019-07-06 19:03:15

    Biashara ya China na Afrika imeongezeka katika miezi mitano ya mwanzo mwaka huu.

    Takwimu zilizotolewa na Mamlaka Kuu ya Forodha ya China zinaonyesha kuwa thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 84.76 katika kipindi hicho, kiasi kilichoongezeka kwa asilimia 3 kuliko mwaka jana wakati kama huo, licha ya biashara ya jumla ya China na nchi za nje zilizofungwa kwa dola za kimarekani kushuka kwa asilimia 1.6 katika kipindi hicho.

    Mwaka jana, thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 204.2, kiasi ambacho kiliongezeka kwa asilimia 20 kuliko mwaka juzi, na China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 10 mfululizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako