• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KOMBE LA DUNIA: Warembo wa Marekani wavikwa taji baada ya kuwashinda Waholanzi kwa 2-0

  (GMT+08:00) 2019-07-08 14:06:00

  Tunaambiwa ladies first hivyo naanza na kipute cha kombe la dunia la wanawake, ambapo jana usiku ilikuwa fainali ya kombe hilo iliyoshuhudia warembo wa Marekani wakiweka rikodi mara nne kwa kuvikwa taji baada ya kuibanjua Uholanzi kwa magoli 2-0. Mabingwa hao watetezi wameshinda katika kipindi cha pili baada ya Megan Rapinoe kupata penalti na kuwalaza chali waholanzi baada ya kipindi cha kwanza kumenyana bila ya kuondoka na goli. Uholanzi ambao ni mabingwa wa Kombe la Ulaya, wamefikia fainali kwa mara ya pili sasa, lakini Marekani imecheza fainali kwa mara ya tatu mfulululizo, ikiendeleza utawala wake wa huko nyuma baada ya kunyakuwa ubingwa katika mwaka 1991, 1999 na 2015. Goli la Rapinoe pia limemfanya ashinde Kiatu cha dhahabu baada ya kumaliza akiwa na magoli sita na ya usaidizi matatu, na pia kueondoka na tuzo ya Mpira wa dhahabu kwa kuwa mchezaji bora.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako