• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Sharks yairarua Everton mbele ya mashabiki wao 64,000

    (GMT+08:00) 2019-07-08 14:06:55

    Wenyeji Kariobangi Sharks walijikakamua mbele ya mashabiki wao na kulemea mabingwa mara tano wa Kombe la FA Everton kutoka nchini Uingereza 4-3 kwa njia ya penalti katika makala ya tatu ya SportPesa Trophy katika uwanja wa Kasarani uliofurika mashabiki wapatao 64,829, jana Jumapili. Muda wa kawaida ulitamatika kwa 1-1 baada ya Duke Abuya kufungia Sharks katika kipindi cha kwanza naye Joe Williams akajaza bao la Everton mapema katika kipindi cha pili. Katika upigaji wa penalti, kipa Brian Bwire alipangua penalti mbili na pia kufunga ya ushindi. Timu zote mbili zilianza vibaya kupiga penalti baada ya Willams na Abuya kupoteza. Nathan Broadhead, Josh Bowler, Fraser Hornby walifunga penalti zao tatu zilizofuata, huku Sharks ikifunga penalti tatu kabla ya Bwire kupangua penalti ya Dennis Adeniran na kisha kufuma ya ushindi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako