• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matumizi ya watu yahimiza maendeleo ya uchumi nchini China

  (GMT+08:00) 2019-07-08 16:34:49

  Takwimu mpya zilizotolewa na Idara kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, katika miaka 70 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, kipato cha wananchi wa China kimeongezeka kwa mfululizo, huku kiwango chao cha matumizi kikiinuka siku hadi siku. Kwa mujibu wa takwimu hizo, mwaka jana wastani wa matumizi ya kila mchina yalizidi dola 2,880 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la mara 19.2 ikilinganishwa na mwaka 1978.

  Takwimu hizo zinaonesha kuwa, wakati Jamhuri ya Watu wa China ilipoanzishwa, kipato na kiwango cha matumizi ya wachina kilikuwa cha chini sana. Mwaka 1956, wastani wa kipato cha mchina ulikuwa dola 37.7 za kimarekani, ambapo wastani wa matumizi ya kila mtu ulikuwa dola 33.8. Baada ya China kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, maendeleo ya kasi ya uchumi yalihimiza ongezeko la kipato cha watu. Mwaka jana, wastani wa kipato cha mchina ulifikia karibu dola 4,100 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la mara 24.3 ikilinganishwa na mwaka 1978. Wakati huohuo, wastani wa matumizi ya kila mchina yalizidi dola 2,880 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la mara 19.2 ikilinganishwa na mwaka 1978.

  Hivi sasa kutokana na ongezeko la kipato, utalii imekuwa njia ya wachina wengi ya kutumia siku za mapumziko. Mkazi moja wa Bejing anasema,

  "Maonesho ya kilimo cha bustani yanafanyika hapa Beijing, tutaenda kutembelea pamoja na mtoto wetu. Aidha, mtoto wetu anapenda opera ya Kunqu, hivyo tumenunua tiketi ili kutimiza matumaini yake."

  Takwimu zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, mwaka jana, mauzo ya jumla ya bidhaa nchini China yalizidi dola trilioni 5.53 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 9 ikilinganishwa na mwaka 2017. Meneja mkuu wa Kampuni ya Mauzo ya Bidhaa ya Mtandaoni Bw. Dan Jiaocheng anasema,

  "Bidhaa zetu nyingi zimeisha. Matunda ya cherry tuliyoagiza kutoka nchi za nje yamependwa sana na wateja, hata watu kutoka miji midogo na vijiji wanayanunua kupitia tovuti yetu."

  Waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan amesema, mahitaji ya soko ni rasilimali muhimu duniani, hivyo kumiliki soko kubwa ni nguvu kubwa zaidi ya kiuchumi ya China. Anasema,

  "Ni lazima tufanye vizuri mambo matatu, kwanza ni kuhimiza matumizi ya watu mijini, na kutoa huduma ya kupata bidhaa ndani ya dakika 15, pili ni kuhimiza matumizi ya watu wanaoishi vijijini, kuwapelekea bidhaa za viwanda, na kuwasaidia kuuza bidhaa za kilimo, na tatu ni kuendeleza sekta ya huduma."

  Mwaka jana wastani wa pato la taifa GDP kwa kila mtu nchini China ulifikia dola 9,732, ambalo ni la juu kuliko kiwango cha nchi zenye pato la kati. Aidha takwimu zinaonesha kuwa, mwaka jana, mchango wa matumizi kwa ongezeko la uchumi nchini China ulifikia asilimia 76.2, na matumizi yamekuwa nguvu kuu ya ukuaji wa uchumi wa China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako