• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makamu wa rais wa China ahutubia kongamano la 8 la amani duniani

    (GMT+08:00) 2019-07-08 18:33:32

    Makamu wa rais wa China Bw. Wang Qishan ameshiriki kwenye kongamano la 8 la amani duniani lenye kauli mbiu ya "kutuliza utaratibu wa kimataifa kushirikiana, kusimamia na kunufaika kwa pamoja" , lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Tsinghua.

    Bw. Wang amesema, maendeleo ya China yanahitaji msaada wa dunia, ambapo maendeleo ya dunia pia yanahitaji mchango wa China. Amesema China itaendelea kufuata njia ya maendeleo ya amani na kutarajia kulinda msingi wa uhusiano wa pande nyingi, kupanua njia za maendeleo ya pamoja na kuhimiza mawasiliano ya utamaduni ili kushirikiana kukabiliana na changamoto za pamoja kwa binadamu.

    Bw, Wang pia amesema China imetoa wito nchi mbalimbali kuzingatia nia ya maendeleo ya amani, kusukuma mbele utandawazi, ili kujenga kwa pamoja utaratibu wenye utulivu na ulio wa haki na ufanisi zaidi wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako