• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa Brexit wa Uingereza asema nchi hiyo itajitoa kwenye Umoja wa Ulaya mwezi Oktoba bila ya kucheleweshwa zaidi

    (GMT+08:00) 2019-07-09 08:39:03

    Waziri wa Uingereza anayeshughulika na Brexit Stephen Barclay amesema, nchi hiyo inapaswa kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya Oktoba 31 mwaka huu, bila ya kuchelewa zaidi, akisisitiza kuwa pande zote mbili zinatakiwa kufanikisha hilo kwa kufikia makubaliano.

    Akizungumza jijini London, Bw. Barclay amesema hatua hiyo ni muhimu kwa maslahi ya pande hizo mbili, na kupinga kufanyika kwa kura ya maoni kwa mara ya pili kuhusu Brexit, akisema kuna baadhi ya wakati hatua hiyo inaeleweka vibaya.

    Siku ya mwisho kwa Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya iliahirishwa kutoka March 29 mwaka huu hadi Oktoba 31, ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu baada ya Waingereza kupiga kura ya maoni ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako