• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Serikali yatoa onyo kwa watoroshaji madini.

    (GMT+08:00) 2019-07-09 18:23:29
    Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewataka watoroshaji wa madini hapa nchini kuacha tabia hiyo mara moja na kusisitiza anaendelea kufuatilia nyendo zao ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

    Akizungumza katika Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, (DiTF), katika Jukwaa la Madini Kuhusu Fursa na Changamoto katika Sekta ya Madini, alisema hawatamtumbia macho mtoroshaji wa madini. Anasisitiza kwamba kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Naibu Waziri anasema bado kuna utoroshaji wa madini lakini wanaendelea kupambana nao kwakuwa wanachangia kudidimiza uchumi wa nchi.

    Madini mengi yamekuwa yakiendelea kupotea ardhini kwa sababu ya ukosefu wa vifaa vya kisasa. Kutokana na vitendo hivyo, alitoa onyo kwa wanaoendesha kampeni ya kukamata watoroshaji hao kuacha kutekeleza agizo hilo kwa upendeleo. Alisema Serikali inahitaji fedha kutoka sekta ya madini, na hivyo wizara ya Madini itafanya chochote kulainisha mambo. Lengo la serikali ni kukusanya Sh bilioni 470 ambapo hapo awali shilingi bilioni 328 zilikusanywa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako