• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Waajiri wasiojisajili fidia waonywa

    (GMT+08:00) 2019-07-09 18:23:50
    Mfuko wa Fidia kwa Wafanyikazi(WCF) umewaomba waajiri ambao bado hawajajisajili na mfuko huo kufanya hivyo ili kuwasaidia wafanyikazi wao kupata fidia wanapopatwa na matatizo kazini. Wito huu umetolewa na mkurugenzi wa Huduma za Tathmini wa WCF, katika maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam.

    Lengo la mfuko huo ni kushughulikia masuala ya fidia kwa wafanyikazi waliopo katika sekta rasmi ya umma na binafsi Tanzania Bara, ambao hupata matatizo ya kuumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi wanazozifanya kwa mujibu wa mikataba hiyo. Kufikia sasa asilimia 85 ya waajiri wakubwa wamejisajili na mfuko huo, huku waajiri wadogo waliojisajili wakiwa asilimia 75.

    Mfuko wa Fidia kwa Wafanyikazi ni taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoundwa kwa mujibu wa sheria,kifungu cha 5 cha sheria ya Fidia kwa Wafanyikazi, sura ya 263, marejeo ya mwaka wa 2015, na kwamba kujisajili ni muhimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako