• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • VOLLEYBALL: Kenya yaibana mbavu Algeria kwenye michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika

    (GMT+08:00) 2019-07-10 10:58:49

    Timu ya taifa ya wanawake ya volleyball ya Kenya, Malkia Strikers, jana jioni ilianza kampeni yake ya kuweka rikodi kwenye michuano ya 10 ya Kombe la mataifa ya Afrika kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Algeria kwenye mechi ya kundi 'B' iliyochezwa uwanja wa October 6 huko Giza, Misri. Awali kwenye kiwanja hichohicho, mabingwa watetezi Cameroon waliwaonesha Botswana umwamba wao kwa kuwachabanga 3-0 kwenye mechi ya ufunguzi wa mashindano yanayoshirikisha timu saba. Kenya, ikiwa chini ya Muitaliana Shaileen Ramdoo, walianza kudhibiti mchezo toka mechi inaanza, na hawakutulia hadi walipofanikiwa kuwabana mbavu Algeria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako