• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Paul Pogba na Jesse Lingard waingia kwenye malumbano

    (GMT+08:00) 2019-07-10 10:59:43

    Nyota wa Manchester United Paul Pogba na mshambuliaji wa timu hiyo Jesse Lingard, walionekana kwenye mfarakano jana Jumanne wakati timu hiyo ilipowasili nchini Australia kujifua kwa msimu mpya wa 2019/20. Kwenye video iliyosambaa katika akaunti ya Twitter ya timu hiyo, Pogba na Lingard walionekana wakikemeana kuhusu suala ambalo bado halijabainika. Wawili hao walionekana wakitembea na kukaribiana kabla ya Lingard kurusha mikono yake hewani kwa hasira akielekea kwa Pogba. Tukio hilo lilifanyika wakati vijana wa kocha Ole Gunnar Solskjaer walikuwa wakitembea na kupunga unyunyu baada ya safari ya saa sita kutoka jiji la Manchester hadi mji wa Perth nchini Australia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako