• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yadumisha utulivu wa bei ya bidhaa

  (GMT+08:00) 2019-07-10 19:08:55

  Takwimu zilizotolewa leo na idara kuu ya takwimu ya China zinaonesha kuwa, mfumuko wa bei nchini China kwa mwezi Juni ulikuwa asilimia 2.7, huku bei ya bidhaa za viwanda ikipungua kwa asilimia 0.3. Wataalam wamesema kiwango cha mfumuko wa bei nchini China kinadhibitika, na bei ya bidhaa itaendelea kwa utulivu.

  Hivi karibuni, ongezeko la bei ya matunda lilifuatiliwa sana na watu. Takwimu zilizotolewa na idara kuu ya takwimu ya China zinaonesha kuwa, kwa mwezi Juni, bei ya matunda mabichi iliongezeka kwa asilimia 42.7, na bei ya nyama iliongezeka kwa asilimia 14.4 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Hata hivyo bei ya jumla ya chakula ilipungua kwa asilimia 0.3 ikilinganishwa na mwezi Mei. Mtafiti wa ofisi ya washauri ya Baraza la Serikali la China Bw. Yao Jingyuan amesema, kutokana na sababu ya majira na homa ya nguruwe, mfumuko wa bei umeendelea kuzidi asilimia 2. Anasema,

  "Tukitaka kujua mabadiliko ya bei ya muda mrefu na wa kati, tunalinganisha bei ya miaka tofauti, na tukitaka kujua mabadiliko ya muda mfupi, tunalinganisha bei ya mwezi huu na mwezi uliopita. Sasa tunaweza kutambua ongezeko la bei ya bidhaa halitaendelea mwezi ujao. Katika nusu ya pili ya mwaka huu, bei ya bidhaa inahakikishwa kuendelea kwa utulivu."

  Idara kuu ya takwimu pia imetoa takwimu kuhusu bei ya bidhaa za viwanda. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, bei hiyo iliongezeka kwa asilimia 0.3 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, lakini kwa mwezi Juni, bei hiyo ilishuka kwa asilimia 0.3 ikilinganishwa na mwezi Mei. Hali hii inatokana na kushuka kwa bei ya mafuta kwenye soko la kimataifa. Mtafiti wa ofisi ya utafiti wa mambo ya jumla ya uchumi ya kituo cha utafiti wa maendeleo cha baraza la serikali la China Bw. Zhang Liqun anasema,

  "Bei ya bidhaa za viwanda ilishuka mwezi Juni. Hali hii inaonesha kuwa pengo la uzalishaji na mahitaji linaendelea kuongezeka. Hili ni suala linalostahili kufuatiliwa na viwanda vyetu haswa vile vidogo na vyenye ukubwa wa kati."

  Bw. Zhang amesema mwelekeo wa bei ya viwanda unahusiana na sera za serikali, endapo China ikiimarisha sera ya kupunguza uzalishaji, na kuhimiza mahitaji ya ndani, bei hiyo inatarajiwa kuongezeka katika nusu ya pili ya mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako